KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, December 14, 2010

David Coltart AAGIZWA KUFANYWA KWA UCHUNGUZI.


Waziri wa michezo nchini Zimbabwe, David Coltart, amelitaka jeshi la polisi nchini humo kufanya uchunguzi wa sababu zilizopelekea upangaji wa matokeo mabovu ya timu ya taifa ya nchi hiyo The Warriors.

Wito huo kwa jeshi la polisi umetolewa na David Coltart, huku miezi kadhaa ikiwa imepita baada ya kitendo cha upangaji wa matokeo kujitokeza baada ya timu ya taifa ya Zimbabwe ilipofanya ziara ya barani Asia na kucheza na timu za taifa za Thailand pamoja na Malaysia.

Waziri huo wa michezo nchini Zimbabwe amefiki hatua ya kulitaka jeshi la polisi kuchukua hatua hiyo kufuatia raisi wa chama cha soka nchini humo Cuthbert Dube kuvieleza vyombo vya habari kwamba mpaka sasa hakuna lolote lililofanyiwa uchunguzi kubaini nini chanzo cha upangaji huo wa matokeo.

Hata hivyo raisi huyo wa ZIFA amesema kilichofanyika mara baada ya kubaini kulikuwepo na upangaji wa matokeo ni kutimuliwa kazi kwa mtendaji mkuu wa chama cha soka Henrietta Rushwaya, ambae alikua mkuu wa msafara wa kuelekea katika nchi za Thailand pamoja na Malaysia walipokwenda kucheza michezo ya kimataifa ya kirafiki.

Amesema kilichobainika ni kwamba Henrietta Rushwaya aliushurutisha uongozi wa ZIFA kukopa dola za kimarekani 10, 3000 kwa ajili ya kufanyika kwa ziara hiyo na alipofanikiwa, alishiriki kukiita kikosi cha klabu ya Monomotapa kama timu ya taifa ya Zimbabwe.

Pamoja na waziri wa michezo kuwa na wazo zuri la kutaka kujua nini kilichosababisha udanganyifu huo, bado nchi ya Zimbabwe huenda ikajikuta ikiingia kwenye matatizo makubwa na shirikisho la soka duniani FIFA ambalo halitaki masuala la soka yaigiliwe na serikali ya nchi mwanachama.

No comments:

Post a Comment