KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, December 14, 2010

USHOGA NA ULEVI MARUFUKU 2022 - Sepp Blatter .


Raisi wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amewataka mashabiki wa mchezo huo wenye tabia za ushoga kufuata sheria za mataifa ya Falme za kiarabu ambapo nchi ya Qatar ambayo ni moja ya nchi hizo imekua mshindi wa kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022.

Sepp Blatter ametoa ushauri huo kwa mashabiki wenye tabia za ushoga kufuatia swali aliloulizwa na mmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa jana uliofanyika nchini Afrika kusini ambapo FIFA walikuwa wakitoa shukurani kwa kamati kuu ya maandalizi ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2010.

Amesema nchi za falme za kiarabu zina utamaduni wa kutokukubaliana na tabai za ushoga na wao kama FIFA hawawezi kuingilia hilo zaidi ya kuwataka wahusika kuachana na tabia zao kwa muda watakaokwenda kutazama fainali za kombe la dunia za mwaka 2022.

Amesema mchezo wa soka hauna kasumba ya kumtenga yoyote kwa kabila, rangi ama tabia lakini mchezo huo una kasumba ya kuheshimu mazingira pasipo kuvunja taratibu zilizowekwa.

Sepp Blatter pia akatio onyo kwa mashabiki wenye tabia ya ulevi kuvumilia tabia hiyo kutokana na nchi ya Qatar kutokukubaliana na utaratibu kuuza vinywaji vya ulevi kama ilivyo kwenye nchi nyingine ambazo tayari zimeshawahi kuandaa fainali za kombe la dunia.

Wakati huo huo raisi huyo wa FIFA ameonyesha kuchukizwa na fununu za baadhi ya watu ambazo zinaeleza kwamba shirikisho hilo limecheza mchezo mchafu wa kupokea rushwa ambayo inadaiwa kuiwezesha nchi ya Qatar kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022.

Blatter amesema fununu hizo ni za kipuuzi na amewataka mashabiki wa soka duniani kuelewa kwamba kwa sasa FIFA wanataka kupanua wigo wa fainali za kombe la dunia ambazo tayari zimeshachezwa katika mabara yote na wanataka ziechezwe sehemu nyingine ambazo hazikuwahi kuchezwa kwa lengo la kuhusishwa tamaduni mbali mbali.

No comments:

Post a Comment