Wakala wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ufaransa Hatem Ben Arfa amesema mchezaji huyo yu mbioni kurejea kwenye kikosi cha klabu ya Newcastle Utd ambacho kwa sasa kipo chini ya meneja mpya Alan Pardew.
Simon Stainrod wakala wa mchezaji huyo, amesema kwa sasa hali ya Hatem Ben Arfa alievunjika mguu mwezi wa kumi mwaka huu inaridhisha na muda si mrefu ataanza mazoezi mepesi ambayo yatamuwezesha kurejea kwenye hali yake ya kawaida.
Simon Stainrod amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ameonyesha matumaini ya kupona haraka mbali na ilivyokua inafikiria hapo awali, hatua ambayo ameitaja kuwa nzuri kwa Hatem Ben Arfa pamoja na kwa viongozi wa klabu ya Newcastle Utd.
Wakati huo huo meneja wa klabu ya Newcastle Utd Alan Pardew amerejesha salam huko White Hert Lane yalipo makao makuu ya klabu ya Tottenham Hotspurs ambapo mapema hii leo zilielezwa taarifa ambazo zilidai klabu hiyo ya jijini London inajipanga kumsajili mshambuliaji wa kiingereza Andy Carroll.
Alan Pardew amerejesha salamu hizo huku akitoa msisitizo wa kutokua tayari kumuuza Andy Carroll ambae tayari ameshazifumania nyavu mara 10 kwenye michuano ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
Amesema litakua jambo la kipuuzi kwa yeye binafsi kukubali kumuachia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, huku ikifahamika yeye ndie shujaa wa mara kwa mara ambae amekua akisaidiana na wachezaji wengine kikosini kuleta ushindi.
Mapema hii leo Spurs walijinadi hadharani kuwa tayari kumtoa mshambuliaji wao Pater Crouch sambamba na kiasi cha fedha kwa ajili ya kumsajili Andy Carroll katika kipindi cha dirisha dogo la usajili kitakachoanza mwanzoni mwa mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment