KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, December 21, 2010

TUNASHUKURU KUMALIZA MZOZO DHIDI YA Carlos Tevez.


Meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini amekua muwazi kwa kueleza ni vipi alivyofarijika mara baada ya kufanikiwa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez, ambae siku za hivi karibuni alizusha songombingo la kutaka kuondoka huko City Of Manchester.

Mancini ameonyesha uwazi huo alipozungumza na vyombo vya habari mara baada ya mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo ambao ulishuhudia kikosi cha Man city kikicheza nyumbani dhidi ya Everton.

Amesema jambo kubwa la kushukuru ni kumaliza mzozo uliokuwa unaendelea kati ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 dhidi ya uongozi wa klabu ya Man City hivyo ni faraja kwa kila mmoja klabuni hapo kwa hatua ya kuanza upya maisha ya maelewano.

Katika mazungumzo hayo Carlos Tevez, alitoa ahadi ya kuendelea kubaki Man City kama mkataba wake unavyoeleza na hii ilikua ni muda mchache kabla ya kuanza kwa mpambano huo wa jana ambao ulimalizika kwa Everton kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Katika hatua nyingine meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia ameonyesha masikitiko kufuatia kikosi chake kushindwa kukwea kwenye kilele cha msimamo wa ligi katika kipindi hiki cha msimu wa sikuku ya X-Mass na mwaka mpya.

Amesema kwa mara ya mwisho kikosi cha Man city kilifanikiwa kukaa kileleni katika kipindi kama hiki mwaka 1929, sawa na miaka 80 hivyo kushindwa katika dhamira hiyo kwake limekua pigo kubwa.

Wakati Mancini akionyesha huzuni baada ya kikosi chake kushindwa kufanya kweli, meneja wa klabu ya Everton David William Moyes, yeye alionyesha furaha alipozungumza na vyombo vya habari kufuatia kikosi chake kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

David William Moyes amesema ni faraja kubwa kwao kupata ushindi wa ugenini tena katika dakika za mwanzoni mwa mchezo ambapo ameainisha kwa kueleza kwamba harakati hizo zimesababishwa na uharaka wa wachezaji wake ambao walionyesha kuwa na hamu ya ushindi.

Meneja huyo toka nchini Scotland pia akazungumzia kufurahishwa na bao la pili lililofungwa na Leighton John Baines, lakini akaonyesha masikitiko ya kutokufurahishwa na adhabu ya kadi nyekundu iliyomkuta mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Nigeria Victor Chinedu Anichebe baada ya kumzuia kipa wa Man City Joe Hart.

No comments:

Post a Comment