KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 15, 2010

INTER MILAN WAIFUATA MAZEMBE FAINALI.



Mabingwa wa soka toka barani Ulaya wamefanikiwa kutinga kwenye hatua ya fainali ya kombe la klabu bingwa duniani baada ya kuwatandika mabingwa wa soka toka barani Asia Seongnam Ilhwa mabao matatu kwa sifuri.

Ushindi huo unawafanya mabingwa hao wa barani Ulaya kuanza maandalizi ya kupambana na mabingwa wa soka toka barani Afrika TP Mazembe ambao wao walitangulia kutinga fainali kufuatia kisago walichokitoa kwa mabingwa wa soka toka barani Amerika kusini Internacioanal.

Mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya kombe la dunia kwa vilabu inatarajiwa kuchezw3a mjini Abu Dhabi siku ya jumamosi.

No comments:

Post a Comment