Meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson amedai haogopi kutimuliwa kazi ndani ya klabu hiyo ambayo kwa sasa inasaka mikakati ya kurejea katika hali ya ushindani kama ilivyokua siku za nyuma.
Roy Hodgson ametoa msisitizo huo huku akionyesha kujiamini alipokua akizungumza na waandishi wa habari juu ya mchezo wa hii leo ambapo Liverpool watakua nyumbani wakicheza na FC Utrecht kwenye michuano ya ligi ya bara la Ulaya.
Amesema anajiamini bado ni mtu muhimu ndani ya Liverpool, pia anaamini mabosi wake wanaimani ana uwezo wa kuendeleza kusaka mipango ambayo itawarejesha kwenya hatua za ushindani na kuondokana na jinamizi la kupoteza michezo kila kukicha.
Alipoulizwa nini malengo ya vikao alivyokua akikutana na mabosi wake mara baada ya kupoteza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita mbele ya Newcastle Utd, mzee huyo mwenye umri wa miaka 63, amesema hakukuwa na vikao kama inavyoelezwa na vyombo vya habari, huku akiwataka waandishi hao kutambua yeye ni meneja anae aminiwa kupitia kazi yake.
Katika hatua nyingine Roy Hodgson amezungumzia mchezo wa hii leo ambapo amesema wanatarajia kuingia katika uwanja wao wa nyumbani huku wakiwa na wazo la kupata ushindi ambao utawaongezea chachu ya kufanya vyema kwenye mchezo yao ijao hususan mchezo wa mwishoni mwa juma hili.
Amesema hawana budi kusahau yaliyopita na kufikiria yaliyo mbele yao ambayo ni mazito zaidi ya yale yaliyojitokeza katika baadhi ya michezo iliyoshuhudia wakipoteza point mbili ama tatu.
Liverpol tayari wameshashanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano ya michuano ya ligi ya barani Ulaya kufuatia kujikusantia point 9 ambazo zinaifanya klabu hiyo kuliongoza kundi la 11 lenye klabu za Steaua Bucharest, Napoli pamoja na FC Utrecht.
Michezo mingine ya ligi ya barani Ulaya itakayochezwa hii leo ni pamoja na:
AZ Alkmaar v BATE Borisov
Club Bruges v Villarreal
Dinamo Zagreb v PAOK Salonika
Dynamo Kiev v FC Sheriff Tiraspol
Lausanne Sports v Palermo
Sparta Prague v CSKA Moscow
Besiktas v Rapid Vienna
FC Porto v CSKA Sofia
Karpaty Lviv v Paris SG
Napoli v Steaua Bucharest
Sevilla v Borussia Dortmund
No comments:
Post a Comment