Mashabiki wa majogoo wa jiji Liverpool wametakiwa kuwa watulivu na kumpa muda meneja wa kikosi chao Roy Hodgson alie na wakati mgumu wa kuirejesha klabu hiyo kwenye mtiririko wa ushindi kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Rai hiyo kwa mashabiki wa Liverpool imetolewa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Kenny Dalglish ambapo amesema anatambua kwa sasa ni wakati mgumu kwa mashabiki kuwa na hali ya uvumilivu na meneja huyo lakini inawalazimu kufanya hivyo kwa lengo la kumpa muda wa kutosha.
Amesema kipindi hiki ni kigumu kwa kila mtu klabuni hapo lakini uvumilivu na subra ni jambo zuri ambalo litamuwezesha Roy Hodgson kujipanga upya na kutazama ni vipi kikosi chake kitaweza kuondokana na dhoruba zito linalowakabili.
Akitolewa mfano wa klabu ya Spurs Kenny Dalglish amedai klabu hiyo nayo imekua katika kipindi kizito cha kupoteza michezo muhimu msimu huu lakini utulivu wa mashabiki wake unaifanya kuwa katika hali zuri ambayo hii leo inawawezesha kushinda.
Rais hiyo kwa mashabiki wa klabu ya Liverpool imetolewa kufuatia kikosi cha The Reds kupoteza mchezo wake wa mwishoni mwa juma lililopita mbele ya Newcastle Utd ambao waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja.
No comments:
Post a Comment