KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, December 13, 2010

ZAMA ZA KUPOTEZA ZIMEKWISHA - Carlo Ancelotti .


Meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti amesema anaamani kikosi chake kinarejea katika njia sahihi ya ushindi baada ya kulazimisha sare ya bao moja kwa moja katika mchezo wa jana uliowakutanisha na Tottenham Hotspurs waliokua nyumbani huko White Hert Lane jijini London.

Carlo Ancelotti ameiweka wazi imani hiyo alipoazungumza na vyombo vya habari ambapo amedai kikosi chake kwa ujumla jana kimeonyesha ushindani zaidi ya michezo iliyopita ambayo imeshuhudiwa wakitoka kappa ama iwe kufungwa au kupata matokeo ya sare.

Sababu kubwa ya kudai kikosi chake kimeonyesha njia ya kureja katika mafanikio, ni kufuatia kurejea kwa baadhi ya wachezaji wake ambao jana kwa asilimia kubwa aliwatumia hali ambayo amedai itawaongezea chachu wachezaji wengine ambao walionyesha kuhitaji usaidizi kutoka kwa wale waliokua nje wakiuguza majeraha.

Wakati huo huo Anceloti ametetea maamuzi ya Didier Drogba kupiga mkwaju wa panati katika dakika za lala salama za mchezo wa jana ambapo amesema mshambuliaji huyo alistahili kupiga mkwaju huo kutokana na mpigaji wa kila siku Frank Lampard kutokuwa katika kiwango chake.

Amesema Lampard alistahili kupiga mkwaju wa panati uliopatikana lakini ukweli ni kwamba kiungo huyo alikuwa hana mazoezi ya kutosha hivyo ilikuwa vigumu kuchukua jukumu lake ambalo mara kadhaa amekua akilitimiza pindi nafasi hiyo inapojitokeza.

Hata hivyo pamoja na Didier Drogba kukosa mkwaju wa panati ambao ulikua muhimu kwao kwa manufaa ya kuibuka na point tatu muhimu, Anceloti amemwagia sifa kem kem mshambuliaji huyo wa kimataifa toka nchini Ivory Coast kwa uwezo mkubwa aliouonyesha ambao ulipelekea kuipatia bao la kusawazisha Chelsea.

No comments:

Post a Comment