Kiungo wa kimataifa toka nchini Ghana Laryea Kingston ametupiwa virago vyake na uongozi wa klabu ya Vitesse Arnhem ya nchini uholanzi.
Laryea Kingston ametupiwa virago vyake huko nchini Uholanzi baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miezi sita, ikiwa ni sehemu ya mkataba wake wa mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo amesema wameamua kuachana na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, baada ya kushindwa kuonyesha uwezo wake wa kiuchezaji kama ilivyokua wakimtumainia wakati wakiingia nae mkataba.
Amesema wakati wakimsajili kutoka nchini Scotland alipokua akiitumikia klabu ya Heart alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu, lakini cha kushangaza alipofika huko Eredivisie alibadilika na kushindwa kuonyesha uwezo kama ilivyokua siku za nyuma.
Mara baada ya mkataba wa Laryea Kingston, kuvunjwa huko nchini Uholanzi, moja kwa moja kiungo huyo alirejea nyumbani kwao nchini Ghana na inasemekana huenda akajiunga na moja ya vilabu vya soka nchini humo.
Laryea Kingston tayari ameshaitumikia timu ya taifa ya Ghana mara 41 na amefanikiwa kufunga mabao 6.
No comments:
Post a Comment