Meneja wa klabu ya Fulham Mark Hughes amekipa saluti kikosi chake kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa sifuri uliopatikana jana dhidi ya Stoke City waliokua nyumbani huko Britannia Stadium.
Hughes, amesema kwa ujumla wachezaji wake walicheza vizuri tena kwa kujituma zaidi na suala hilo limekua na mafanikio mazuri ya kupata ushindi ambao umewawezesha kufikisha point 19 ambazo zimewaondosha kwenye mstari wa kushuka daraja msimu huu.
No comments:
Post a Comment