Shirika la utangazaji nchini Uingereza BBC hii leo linatarajia kumtangaza mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika kwa mwaka 2010, baada ya kutoa wachezaji walioingia kwenye hatua ya fainali ya kinyang’anyiro hicho.
BBC wanatarajia kumtangaza mshindi wa tuzo hiyo, kwenye hafla itakazofanyika mjini Cairo nchini Misri baada ya mashabiki wa soka ulimwenguni kote kuhusishwa na hatua ya kuwapigia kura wachezaji waliingia hatua ya fainali kupitia njia ya mtandao wa Internet.
Wachezaji waliotangazwa kuingia kwenye hatua ya fainali ya kinyang’anyiro cha kuwani tuzo ya mchezaji bora wa BBC wa bara la mwaka 2010 ni Asamoah Gyan pamoja na Andre 'Dede' Ayew (Ghana), Samuel Eto'o (Cameroon), Yaya Toure pamoja na Didier Drogba (Ivory Coast).
Tuzo hiyo kwa mwaka jana ilichukuliwa na Didier Drogba (Ivory Coast)
2008 - Mohamed Aboutrika (Misri)
2007 - Emmanuel Adebayor (Togo)
2006 - Michael Essien (Ghana)
2005 - Mohamed Barakat (Misri)
2004 - Jay-Jay Okocha (Nigeria)
2003 - Jay-Jay Okocha
2002 - El Hadji Diouf (Senegal)
2001 - Sammy Kuffuor (Ghana)
2000 - Patrick Mboma (Cameroon)
No comments:
Post a Comment