Shirikisho la soka barani Ulaya hii leo limetangaza ratiba ya hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani humo huku baadhi ya michezo iliyochezwa msimu uliopita ikijirudiwa kwa asilimia kubwa.
Shughuli za upangaji wa ratiba hiyo zimeendeshwa kwenye ukumbi wa mikutano wa UEFA na katibu mkuu wa shirikisho la soka barani Ulaya Gianni Infantino kwa kushirikiana na wadau wengine wa soka toka barani humo.
Roma v Shakhtar Donetsk
AC Milan v Tottenham Hotspur
Valencia v Schalke
Inter Milan v Bayern Munich
Lyon v Real Madrid
Arsenal v Barcelona
Marseille v Manchester United
FC Copenhagen v Chelsea
Hatua hiyo ya mtoano itaanza kuunguruma February 15 pamoja na 16 na michezo ya marejeano itakuwa March 22 and 23 mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment