KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, December 28, 2010

MILANGO IWAZI KWA Marcus Nathan Bent.


Meneja wa klabu ya Birmingham City Alex McLeish ameeleza wazi kumfungulia mlango wa kuondokea mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Uingereza Marcus Nathan Bent.

Alex McLeish ameeleza wazi mpango huo mbele ya vyombo vya habari ambapo amesema mshambuliaji huyo ambae kwa sasa anaichezea klabu ya Wolverhampton Wanderers kwa mkopo hana budi kuondoka kufuatia kukosa nafasi katika kikosi chake cha kwanza.

Amesema lengo lake yeye ni kutaka kumpa uhuru Marcus Nathan Bent kucheza kila juma na ndio maana alifanikisha suala la kumpelekea kwa mkopo humo Molinioux Stadium ambapo hata hivyo bado amekosa nafasi ya kutimiza melengo hayo kufuatia mpaka sasa kuambulia kucheza michezo miwiwli tu akiwa na klabu hiyo.

Alex McLeish meneja wa kimataifa toka nchini Scotland alimsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 mwaka 2008 akitokea Charlton Athletics kwa ada ya uhamisho wa Paund Milion moja.

Wakati huo huo Alex McLeish amesema hana shaka hata kidogo juu ya mchezo wa hii leo ambao utawakutanisha na vinara wa msimamo wa ligi ya Uingereza Man Utd ambao wameifunga safari kuelekea huko St Andrews.

Amesema shaka hiyo haipo tena kufuatia kikosi chake kujiandaa vizuri licha ya matatizo ya hali ya hewa yanayoendelea huko nchini Uingereza lakini bado akaonyesha imani ya kutimiza malengo ya ushindi dhidi ya mashetani hao wekundu ambao mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja.

No comments:

Post a Comment