Meneja wa klabu ya Everton David Moyes ameonyesha hali ya kupungukiwa ndani ya kikosi chake kufuatua kuondoka kwa mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Australia Tim Cahil ambae amejiunga na timu yake ya taifa inayoshiriki fainali za mataifa ya barani Asia.
David Moyes ameonyesha dhahiri kupungukiwa na mchezaji muhimu ndani ya kikosi chake, kufuatia yeye mwenyewe binafsi kukiri kwamba Tim Cahil ni mchezaji wa kipekee na mara kadhaa amekua akiiwezesha The Toffees kupata ushindi hivyo kuondoka kwake kunampa wakati mgumu.
Amesema tayari ameshamtaka kiungo wake wa kimataifa toka nchini Hispania Mikel Arteta kulivaa jukumu la usaidiazi wa safu ya ushambuliaji mpaka hapo atakaporejea Tim Cahil, huku akijifariki kwa kueleza kwamba kiungo huyo ataweza kutimiza jukumu hilo alilompa.
Amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 endapo atasaidiana vyema na washambuliaji wengine klabuni hapo kama Louis Saha, Yakubu Aiyegbeni pamoja na Jermaine Beckford kuna uwezekano mkubwa wa kufanikisha malengo ya ushindi kuanzia mchezo wa hii leo ambapo watapambana na West Ham utd huko Upton Park.
Katika hatua nyintgine David Moyes azungumzia kusikitishwa na hatua ya kikosi chake kushindwa kucheza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita ambapo walitakiwa kucheza na Birmingham city.
Amesema tayari alikua ameshakiandaa kikosi chake kwa ajili ya mchezo huo lakini alisikitishwa na hali ya hewa ambayo ilikua chanzo cha mchezo huo kutokufanyika huko Goodson Park.
No comments:
Post a Comment