KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, December 13, 2010

Sepp Blatter AIKUBALIA AFRIKA.


Raisi wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter hii leo ametoa shukurani zake za dhati kwa kamati ya maandalizi ya fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Afrika kusini kuanzia June 11 hadi July 11 mwaka huu huko nchini Afrika kusini.

Sepp Blatter ametoa shukurani hizo akiwa nchini Afrika kusini ambapo amesema kamati hiyo ilifanya kazi nzuri katika maandalizi yake na wao kama FIFA wamefurahishwa na fainali za kombe la dunia zilizochezwa kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika toka kuanzishwa kwake mwaka 1930.

Amesema bado kuna umuhimu wa fainali hizo kuendelea kukumbukwa na waafrika wote kufuatia mambo mengi mazuri kujitokeza mbali na nchi zingine ambazo zimeshawahi kuandaa fainali hizo.

Blatter pia ametoa shukurani zake za dhati kwa raisi wa Afrika kusini, Jacob Zuma ambae ane alikuwepo katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg.

Raisi huyo wa FIFA pia ameonyesha kufurahishwa na ukarimu anaoendelea kuonyeshwa na waafrika ambapo amedai wamekua wakimthamini kutokana na maneno mazuri ya ukaribisho wanayompa popote pale anapokwenda.

Nae raisi wa Afrika kusini Jacob Zuma amezungumzi faida kubwa walizozipata mara baada ya kufanyika kwa fainali za kombe la dunia nchini kwake ambapo amedai kikubwa ambacho kitaendelea kuwanyanyua ni mipango mizuri ya kuendeleza mchezo wa soka.

Amesema hii leo wamebaki na viwanja vyenye viwango vya hali ya juu hatua ambayo anaamini inaibua changamoto mbali mbali kwa wadau wa mchezo huo kujifunza mengi kwa ajili ya kuendeleza soka nchini Afrika kusini na ikiwezekana katika nchi nyingine za bara la Afrika.

No comments:

Post a Comment