KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, December 20, 2010

SIO WA KUWADHARAU HATA KIDOGO.


Aliekua meneja wa mabingwa wa soka nchini Uingereza Chelsea Jose Mourinho amewataka wachezaji wa klabu hiyo kutobweteka baada ya ratiba ya hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa kutolewa mwishoni mwa juma lililopita na kujikuta wameantgukia kwa FC Copenhagen ya nchini Denmark.

Jose Mourinho ambae kwa sasa anakinoa kikosi cha Real Madrid ametoa angalizo hilo kwa wachezaji, kufuatia fununui zinazoendelea miongoni mwa mashabiki wa klabu ya Chelsea ambao asilimia kubwa wamekua wakitamba tayari kikosi chao kimeshapenya na kutinga katika hatua ya robo fainali.

Amesema yeye binafsi anawatambua Fc Copenhagen kuwa ni wazuri hivyo haipaswi kudharaurika kama ilivyo sasa kwa baadhi ya watu wanaoishangilia Chelsea ambayo itaanzia ugenini ana kisha kumaliza nyumbani pindi itakapokutana na wadenmark hao.

Jose Mourinho pia kazungumzia mchezo mwingine wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo Arsenal watakua na kibarua kigumu kwa kucheza na mabingwa wa soka huko nchini Hispania Fc Barcelona.

Amesema Arsenal wanatakia kujishika kweli kweli katika mchezo huo na ifahamike wamelazimika kukutana na Barcelona kufuatia makosa yao waliyoyafanya wenyewe ya kutokufanya vizuri katika hatua ya makundi.

Mourinho pia akakumbushia mchezo wa msimu uliopuita ambao ulishuhudia Arsenal wakilazimisha sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Barcelona lakini wakakiona cha mtema kuni walipofunga safari kuelekea Camp Nou ambapo waliangukiwa na mvua ya mabao manne kwa moja huku mabao manne ya ya Barca yalipachikwa wavuni na Lionel Messi.

Katika hatua nyingine meneja huyo wa kimataifa toka nchini ureno amezungumzia mchezo utakaokihusisha kikosi chake dhidi ya Olympic Lyon toka nchini Ufaransa.

Amesema anatambua olimpic Lyon kwa kipindi cha misimu kadhaa wamekua wakiinyanysa sana Real Madrid pindi wanapokutana nayo, na kufikia hatua ya kuiondosha kabisa mashindanoni, lakini kwa msimu huu ameahidi kurekebisha makosa yaliyokua yakijitokeza misimu iliyopita na ana imani atafanikiwa katika suala hilo.

No comments:

Post a Comment