KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, December 20, 2010

PESA SI LOLOTE KTK SOKA - David Moyes


Meneja wa klabu ya Everton David Moyes amewataka mashabiki wa soka ulimwenguni kote kutambua pesa si lolote si chochote katika mchezo wa soka hivyo inatakiwa itambulike kuwa kinachowezesha mafanikio kwenye mchezo huo ni uwezo wa wachezaji wa klabu husika.

David Moyes amewakumbusha mashabiki wa soka ulimwenguni kote suala hilo, huku yeye pamoja na kikosi chake wakiwa safarini kuelekea mjini Manchester kupambana na Man City, ambao msimu huu wametumia kisi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuwasajili wachezaji wenye hadhi ulimwenguni kote.

Amesema anatambua usiku huu wanakwenda kupambana na klabu iliyotumia zaidi ya paund million 350 zilizotolewa na mmiliki wa klabu hiyo ya City Of Manchester Sheikh Mansour ambae alianza kuimiliki toka mwaka 2008.

Amesema kikubwa wanachokifuata mjini Manchester ni ushindi kama ilivyokua misimu miwiwli iliyopita hivyo hawatojalia wanapambana na kikosi chenye gharama kubwa licha ya kusheheni wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kisoka ambao pia wanakila sifa za kuiwezesha Man city kutwaa ubingwa msimu huu.

Akizungumzia upande wa kikosi chake David Moyes, amebainisha wazi kwamba wapo katika wakati mgumu hasa kipindi hichi cha kuelekea kwenye sikuku hivyo ina walazimu kufanya jitihada zote za kupata point tatu muhimu kila waingiapo uwanjani.

Katika hatua nyingine David Moyes ameshindwa kuzungumzia kwa undani zogo la mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez ambae ametangaza yu tayari kuondoka huko City Of Manchester.

Amesema suala la mchezaji huyo lipo mikononi mwa uongozi wa klabu ya Man City hivyo si shughuli yake kuzungumza, lakini ukweli ni kwamba anamzimikia mshambuliaji huyo toka alipojiunga na klabu ya Man city mwanzoni mwa msimu uliopita.

Wakati huo huo meneja msaidizi wa klabu ya Man City David Platt nae amesema mchezo wa hii leo utakua mgumu kwa pande zote mbili hasa ukizingatia upande wa wapinzani wao wana wachezaji wakali ambao wanatakiwa kuchungwa muda wote na kama itashindikana mambo yatawauwia vigumu.

Amesema mchezaji kama Tim Cahil, mara kadhaa amekua akitumia makosa ya timu pinzani kuiwezesha klabu yake kupata ushindi sambamba na Marouan Felaini ambae anacheza nafasi ya kiungo.

No comments:

Post a Comment