KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, December 27, 2010

TUTAMLINDA DROGBA JICHO KWA JICHO, MGUU KWA MGUU.


Meneja wa jeshi la washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal Arsene Wenger amesema usiku huu safu yake ya ulinzi ina kazi ya ziada ya kumchunga mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivoy Coast pamoja na klabu ya Chelsea Didier Drogba.

Arsene Wenger amekiri kuwepo kwa shughuli hiyo kufuatia ukweli kuendelea kujidhidhirisha wazi kwamba Didier Drogba amekua akiwasumbua sana walinzi wa Arsenal kila wakati hali ambayo imemfanya kujijengea umaarufu mkubwa wa kuzifumania nyavu za klabu hiyo ya kaskazini mwa jiji la London.

Amesema usiku huu Drogba atakua adui yao namba moja na dhamira yao si kumzuia yeye asifunge bali ni kuhakikisha kikosi chake kinaziba mianya mingine ambayo inaweza kuwaletea madhara ambayo huenda yakapeklekea kupoteza point tatu muhimu.

Aidha mzee huyo wa kifaranza ameeleza kuwa, usiku huu ni muhimu kwa kikosi chake kwa kuuthibitishia ulimwengu wa wapenda soka ni vipi walivyo makini katika harakati za kuuwani ubingwa ambao amekiri upo mikononi mwa Chelsea pamoja na Man Utd.

Nae meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Anceloti ameonyesha kuihofia Arsenal ambapo amesema kwa ujumla ina kikosi kizuri chenye uwezo wa kuzuia na kushambulia wakati wote hivyo wanaelekea Emirates usiku huu wakitambua suala hilo.

Anceloti pia akazungumzia ujasiri wa mshambuliaji wake Didier Drogba pale wanapocheza na Arsenal kwa kumueleza kwamba ni mchezaji jasiri na mara kadhaa amekua na akihofiwa na asilimia kubwa ya wachezaji wa The gunners.

Katika mchezo wa usiku huu Arsenal wataendelea kuwakosa baadhi ya wachezaji wao walio majeruhi kama Manuel Almunia, Gibbs (Kifundo cha mguu ), Frimpong (Goti), Vermaelen (Kisigino).

Chelsea wao wataendelea kumkosa Alex (Mguu), Benayoun (kisigino), Zhirkov (kiazi cha mguu)

Arsenal wanaingia uwanjani hii leo huku wakiwa na kumbu kumbu ya kupoteza mchezo wao Uliopita dhidi ya Man utd ambapo siku hiyo walishuka kikosi kilichokua kimesheheni wachezani kaka: Soznisny, Sagna, Koscielny, Squillaci, Clichy, Rosicky (Fabregas 64), Nasri, A Song, Wilshere (Van Persie 64), Arshavin (Walcott 77), Chamakh huku wachezaji wa akiba ambao hawakutumika wakiwa ni: Fabianski, Djourou, Denilson pamoja na Bendtner.

Chelsea wao wanakwenda Emirates huku wakiwa na kumbu kumbu ya matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya (Tottenham,) ambapo katika mchezo huo wachezaji waliotumika ni: Cech, Ferreira, Ivanovic, Terry, Cole, Ramires, Mikel (Drogba 46), Essien, Kalou (Sturridge 68), Anelka, Malouda (Lampard 77).

Wachezaji wa akiba ambao hawakutumika ni: Turnbull, Van Aanholt, Bruma pamoja na McEachran.

No comments:

Post a Comment