KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 16, 2010

VIJANA WAMKOSHA BABU !!


Meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson ameonyesha kufurahishwa na kikosi chake ambacho usiku wa kuamkia hii leo kiliendeleza kasumba ya kutokufungwa na klabu za kutoka nchini Uholanzi.

Hodgson ameonyesha furaha hiyo huku akijivunia kikosi chake ambacho kilikuwa kimesheheni wachezaji chipukizi ambao amedai wameonyesha mustakabali wa klabu ya Liverpool kwa siku za usoni.

Amesema hii ni mara ya pili kukipanga kikosi hicho msimu huu ambapo kwa mara ya kwanza kilicheza dhidi ya Northampton kwenye michuano ya kombe la ligi na jana kilicheza na klabu ya Utrech kwenye michuano ya ligi ya barani Ulaya.

Hata hivyo mzee huyo wa kiingereza amebainisha wazi kwamba licha ya matokeo ya sare kupatikana bado kikosi hicho kilicheza vizuri na kimetimiza lengo la kuiwezesha Liverpool kumaliza michezo ya kundi la 11 ya ligi ya ya barani Ulaya ikiwa katika nafasi ya kwanza.

Wakati huo huo Roy Hodgson ametoa sababu kwa nini hakumchezesha mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando Torres katika mchezo huo ambapo amesema kulikua hakuna sababu ya kumjumuisha kikosini ili hali tayari walikua wameshafuzu kuingia kwenye hatua ya mtoano.

Amesema mshambuliaji huyo ni hazina kubwa kwa michezo kadhaa inayowakabili kwa hivi sasa hivyo ni hatari kumtumia kwenye michezo ambayo haina umuhimu mkubwa ambapo amedia huenda akapata majeraha.

No comments:

Post a Comment