KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 16, 2010

ROVERS WATOA SABABU ZA KUMTIMUA BIG SAM.


Hatimae wamiliki wa klabu ya Blackburn Rovers wametoa sababu zilizopeklekea kumfukuza kazi aliekua meneja wa kikosi cha klabu hiyo Samuel "Sam" Allardyce.

Wamiliki hao wamelazimika kutoa sababu hizo kufuatia uvumi uliokua umetanda katika sehemu mbali mbali ambao ulikua unadai kwamba Sam Allardyce ametimuliwa kazi kufuatia kuchukizwa na utaratibu wa kukataliwa kwa ombi lake la kufanya usajili klabuni hapo kupitia usajili wa dirisha dogo mwezi januari mwaka 2011.

Akifafanua nini kilichopelekea kutimuliwa kazi kwa Big Sam, mwenyekiti wa klabu hiyo ya nchini Uingereza mwana mama Anuradha Desai, amesema Allardyce ameshindwa kuweka wazi mipango ya kuiendeleza Rovers ambayo inatakiwa kudumu leo na kesho kwa kuwa na wachezaji wenye viwango.

Anuradha Desai amedai kwamba mipango yao mikubwa ambayo waliitegemea kutoka kwa meneja huyo ni kuwa na mfumo wa vikosi vya vijana kama ilivyo kwa klabu ya Arsenal lakini suala hilo limeshindikana kwa mzee huyo mwenye umri wa miaka 56.

Amesema klabu ya Blackburn Rovers inatakiwa kubadilika kutoka kwenye mfumo wa zamani na kuingia katika mfumo wa kisasa ambao utawawezesha kuondokana na mfumo wa kumaliza katika nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi, hivyo kuna ulazima wa mipango mipya ikatambulishwa rasmi klabuni hapo.

Hata hivyo mwana mama huyo amewataka mashabiki wa Rovers kuuelewa melengo yaliyowekwa na uongozi mpya wa klabu hiyo ambao unaongozwa na ndugu wawili kutoka nchini India Balaji Rao pamoja na Venkatesh Rao.

Hata hivyo Anuradha Desai ametanabai kwamba maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya Samuel "Sam" Allardyce yalifikiwa kwenye kikao ambacho kimuhusisha Big Sam hivyo alijua nini kinachofuata mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.

Desai pia akaanika wazi kwamba mpaka meneja huyo anaodoka huko Ewood Park hakuwa amewasilisha orodha ya wachezaji aliotaka kuwasajili katika kipindi cha dirisha dogo la usajili, lakini wanategemea kazi hiyo itafanywa na meneja msaidizi Steve Kean.

No comments:

Post a Comment