KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, February 10, 2011

ADEBAYOR AMSIFIA MOURINHO.


Mashambuliaji wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Sheyi Adebayor ameusifia utawala wa meneja wa klabu ya Real Madrid José Mário dos Santos Félix Mourinho ambae alimsajili kwa mkopo akitokea Man City ya nchini Uingereza katika msimu wa dirisha dogo mwezi Januari mwaka huu.

Emmanuel Sheyi Adebayor ameusifia utawala wa meneja huyo wa kimataifa toka nchini Ureno, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika huko Estadio St Bernabeu ambapo amesema Jose Mourinho ni mtu mwenye busara na anafurahishwa na hatua ya kubahatika kufanya nae kazi.

Amesema meneja huyo mwenye umri wa miaka 48, huchukua muda wake mwingi kukaa pamoja na wachezaji wake na kuwaelekeza pale wanapokwenda kinyume na maelekezo yake hatua ambayo kwake amedai ni nzuri na hakudhani kama Mourinho ni mtu wa namna hiyo.

Adebayor mwenye umri wa miaka 26 ameendelea kueleza wazi kwamba kwa mfumo huo alioukuta huko mjini Madrid unamfanya ajisikie mwenye furaha wakati wote anapokua mazoezini na uwanjani kwa ajili ya kuitetea klabu hiyo ambayo imeingia nae mkataba hadi mwishoni mwa msimu huu.

Alipoulizwa juu ya tofauati ziliowahi kujitokeza kati yake na meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini ama wachezaji wenzake wa klabu hiyo Adebayor aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutokuwa mkorofi na mara nyingi anapotimiza wajibu wa kile kilichompelekea barani ulaya watu wengi humtafsiri kuwa tofauti na wenzake.

Amesema alikwenda Ulaya kusaka maisha na wala hakwenda huko kukwaruzana na mtu, hivyo ameomba kutambuliwa kama mchezaji mwema, mwenye nidhamu na mwenye kupenda kucheka na watu wakati wote.

Toka alipojiunga na klabu Real Madrid Emmanuel Sheyi Adebayor ameshajumuishwa kikosni mara tatu na ameshazifumania nyavu mara mbili.

No comments:

Post a Comment