Hatimae mabingwa wa soka nchini Hispania Fc Barcelona wa wametoa tamko rasmi la kujiengua kwenye harakati za kutaka kumsajili kiungo na nahodha wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas mwishoni mwa msimu huu.
Taarifa za kujiengua kwenye harakati hizo zimeelezwa bayana na mkurugenzi wa michezo klabuni hapo Raul Sanllehi ambapo amesema katika mipango yao ya mwishoni mwa msimun huu jina la kiungo huyo halipo na wala hawatojihusisha tena kujadili suala la uhamisho wake.
Amesema kwa sasa wamejipanga vyema kuwatumia wachezaji chipukizi huko Camp Nou hivyo hawaoni umuhimu wa kumrejesha Cesc Fabregas mjini Barcelona kama ilivyokua ikifikiriwa siku za nyuma.
Mwanzoni mwa msimu huu zogo la kusajiliwa kwa kiungo huyo lilitanda kila kona ya ulimwengu lakini yeye binafsi alitangaza kubaki Arsenal kwa mapenzi yake ya dhati baada ya kuwepo klabuni hapo kwa kipindi cha miaka tisa iliyopita.
Hata hivyo kiungo huyo kwa sasa nahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ya Chelsea kwa uhamisho wa paund million 50 ikiwa ni sehemu ya mipangoya mmiliki wake Roman Abramovich.
No comments:
Post a Comment