KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, February 2, 2011

ALISTAHILI KADI, HAKUSTAHILI KADI - ALITUKANA, HAKUTUKANA !!!


Meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Charles Ernest Wenger, amemtetea nahodha na kiungo wa kikosi chake Francesc "Cesc" Fàbregas Soler kufuati meneja wa klabu ya Everton David William Moyes kudai kwamba mchezaji huyo alistahili kuadhibiwa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo huko Emirates Stadium.

Meneja wa klabu ya Everton David William Moyes aliibua madai hayo saa chache baada ya mchezo huo kumalizika ambapo amesema "Cesc" Fàbregas alistahili kupewa adhabu hiyo kufuatia maneno machafu aliyomtamkia muamuzi Lee Mason ambae alilikubali bao la kuotea la The Toffees lililoifungwa na Louis Laurent Saha katika dakika ya 24.

Amesema kiungo huyo wa kimataifa toka nchini Hispania alitamka maneno makali ambayo hayendani na hadhi ya uchezaji wake na alipotakiwa kueleza wazi ni maneno yapi aligoma kuyasema huku akidai hawezi kuyatamka hadharani.

Hata hivyo Moyes amekiri bao lililofungwa na mshambulaiji wake Louis Laurent Saha katika dakika ya 24 lilikua si sahihi kwani mshambuliaji huyo alikua ameotea kabla ya beki wa klabu ya Arsenal kuucheza mpira.

Kufuatia tuhuma hizo Arsène Charles Ernest Wenger amesema nahodha wake hakusema lolote kama inavyodaiwa na Moyes wakati wa mapumziko zaidi ya yeye binafsi kuzungumza na muamuzi Lee Mason kwa kumlalamikia kwa maamuzi aliyoyafanya.

Amesema anastahili kuulizwa kwa undani yeye kama meneja wa klabu ya Arsenal kwani alikua karibu na Fabregas wakati walipokua wakielekea kwenye vyumba vya kupumzika.

Alipoulizwa juu ya bao la Saha mzee huyo wa kifaransa aliungana na meneja mwenzake kwa kusema bao hilo halikua sahihi kwani tayari mshambuliaji huyo kabla ya kufunga alikua ameshaotea.

Katika hatua nyingine Wenger amekipa tano kikosi chake kwa juhudi za kusaka ushindi katika mchezo wa jana ambao tayari ulikua unaonekana huenda wachezaji wake wangepoteza baada ya kusononeshwa na maamuzi ya muamuazi Lee Mason.

No comments:

Post a Comment