Siku chache baada ya aliekua raisi wa nchini Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali kuachia madaraka na kukimbilia uhamishoni nchini Saudi Arabia, hii leo Faouzi Benzarti alieteuliwa kurejea katika madaraka ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo The Carthage Eagles nae amatangaza kuachia ngazi.
Faouzi Benzarti ametangaza kuachia madaraka hayo huku akitao sababu zinazohusiana na kuondoka kwa raisi Zine al-Abidine Ben Ali ambae amedai alikua akitumia mabavu kumshurutisha kuifanya kazi yake.
Akihojiwa na moja ya chombo cha habari nchini Tunisia Faouzi Benzarti amesema ilimlazimu kurejea tena kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tunisia mwezi mmoja uliopita kufuatia amri iliyotolewa ikulu na raisi Zine al-Abidine Ben Ali ambae alimlazimisha kwa nguvu za madaraka aliyokua nayo.
Amesema kuondoka kwa raisi huyo baada ya kushurutishwa na wananchi wa Tunisia ambao walikua wakihitaji uhuru, nae kumempa nafasi ya kujihisi kuwa huru na kuamua kutangaza kuondoka kwenye kazi aliyolazimishwa kuifanya.
Kuondoka kwa Benzarti kumeufanya uongozi wa shirikisho la soka nchini Tunisia kumtangaza Ammar Souayah kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ambayo inakabiliwa na michuano ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 2012.
Hii si mara ya kwanza kwa Ammar Souayah kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tunisia kwani tayari ameshafanya hivyo kwa kukiongoza kikosi cha The Carthage Eagles kilichoshiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2002 zilizochezwa nchini Japan pamoja na Korea kusini.
No comments:
Post a Comment