Uongozi wa chama cha soka nchini Afrika kusini SAFA unaangalia uwezekano wa kubadilisha jina la timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo kwa sasa inajulikana kama Bafana Bafana.
Uongozi wa chama hicho unaangalia uwezekano huo kufuatia haki za jina la Bafana Bafana kushikiliwa na wafanyabiashara wawili nchini Afrika kusini ambao waliibatiza timu ya taifa jina hilo mwaka 1994 kwenye fainali za mataifa ya bara la Afrika zilizochezwa nchini Afrika kuisni.
Tayari uongozi wa SAFA umeshaunda kamati ya watu watatu kwa ajili ya kusaka jina jipya la timu hiyo ambayo ni miongoni mwa mataifa yanayoendelea kusaka mafanikio ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika kwa mwaka 2012.
Kamati hiyo ya watu watatu inaundwa na raisi wa SAFA Kirsten Nematandani, aliekua mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya fainali za kombe la dunia Daniel Alexander "Danny" Jordaan pamoja na mwenyekiti wa kamati ya waamuzi nchini Afrika kusini Alpha Mchunu.
Kamati hiyo inaongozwa na raisi wa chama cha soka nchini Afrika kusini Kirsten Nematandani.
No comments:
Post a Comment