KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, February 11, 2011

Branislav Ivanovic KUBAKI STAMFORD BRIDGE.


Beki wa kimataifa toka nchini Serbia Branislav Ivanovic amesaini mkataba mpya wa klabu ya Chelsea ambao utaendelea kumuweka huko Stamford Bridge hadi mwaka 2016.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 26 amesaini mkataba mpya kufuatia mkataba wake wa hivi sasa kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao, ambapo tayari baadhi ya vilabu vilikua vimeshaanza kujihusisha na utaratibu wa kutaka kumsajili.

Baada ya kukamilisha hatua ya kusaini mkataba mpya klabuni hapo Branislav Ivanovic alikaririwa akisema kwamba ni faraja kubwa kwake kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo hivyo anaamini mchango wake utafanikisha sehemu ya mafanikio yaliyolengwa kufikiwa ndani ya muda huo.

Amesema kwa kipindi cha miaka mitatu aliyokaa huko Stamford Bridge, alijitahidi kucheza kwa kujituma zaidi na hii leo amefanikiwa kuwashawishi viongozi wake kuendelea kuuthamini mchango alioutoa klabuni hapo.

Mpaka sasa Branislav Ivanovic ameshaitumikia Chelsea kwa kucheza michezo 99 na kupachika mabao manne.

No comments:

Post a Comment