Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amesema kikosi chake usiku wa kuakia hii leo kilionyesha umahiri mkubwa wa kucheza na timu yenye uzoefu wa kutumia makosa ya timu pinzani kushinda kirahisi.
Capello ambae alionekana mwenye furaha wakati wote baada ya kikosi chake kupata bao la pili dhidi ya timu ya taifa ya Denmark amesema kila mmoja aliekua anaufuatilia mchezo huo alifurahishwa na upinzani uliokuwepo uwanjani na mwisho wa siku upande wake uliibuka mbabe.
Amesema mchezo huo wa jana pia utawasaidia wachezaji waliokuwepo kikosini katika michezo yao mwishoni mwa juma hili watakapokua kwenye vilabu vyao pamoja na kwenye michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambayo itaunguruma kati kati ya juma lijalo.
Fabio Capello pia akaelezea kuguswa na uwezo mkubwa ulioonyeshwa na wachezaji wake wenye umri mdogo Jack Wilshire pamoja na Asheley Young ambae aliifungia Uingereza bao la pili na la ushindi.
Frank James Lampard aliekiongoza kikosi cha Uingereza jana nae ameonyesha kufurahishwa na ushindi uliopatikana huku akieleza kwamba ushindi huo utawasaidia katika mchezo ujao wa mwezi March mwaka huu.
Amesema wamejifunza mengi kutoka kwa wapinzani wao waliokua nyumbani sambamba na kuguswa na uchezaji wa kinda Jack Wilshire ambae jana amecheza kwa muda wa dakika 90 kwa mara ya kwanza toka alipoanza kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment