Kikosi cha timu ya taifa ya Ghana chini ya umri wa miaka 20 kinatarajia kuweka kambi mjini Barcelona kabla ya kurejea barani Afrika katika kindumbwe ndumbe cha fainali za mataifa ya barani humo zitakazofanyika nchini Libya kuanzia March 18- April 1.
Kikosi hicho cha timu ya taifa ya vijana cha Ghana kitakapokua mjini Barcelona kitafanya maandalizi ya fainali hizo kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu ya Barcelona kuanzia 4-10 March.
Mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana nchini Ghana Jordan Anagbla amesema tayari wameshakubaliana na uongozi wa klabu ya Barcelona juu ya kuwekwa kwa kambi hiyo na wanaamini hatua hiyo itawasaidia kufikia malengo yaliyowekwa mwaka huu.
Amesema mbali na kufanya maandalizi katika viunga vya klabu hiyo bingwa nchini Hispania pia watacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya kikosi cha pili cha klabu ya Barcelona.
Katika michuano ya fainali za mataifa ya bara la Afrika chini ya umri wa miaka 20 timu ya taifa ya Ghana imepangwa katika kundi la pili lenye timu za Nigeria, Gambia pamoja na Cameroon.
Ghana wataanza harakati a wa kuuwania ubingwa fainali za mataifa ya bara la Afrika chini ya umri wa miaka 20 kwa kucheza na timu ya taifa ya Nigeria, March 19.

No comments:
Post a Comment