KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, February 2, 2011

TUSAHAU YALIYOPITA LIVERPOOL IENDELEE.


Meneja wa klabu ya Liverpool King Kenny Dalglish ametoa kauli ya kujifariji baada ya kukubali kuondoka kwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando José Torres Sanz aliejiunga na klabu ya Chelsea usiku wa kuamkia jana.

King Kenny Dalglish ametoa kauli hiyo huku akisema maisha yanastahili kuendelea huko Anfield mara baada ya kukamilika kwa usajili wa mshambuliaji huyo na hadhani kama kuna jambo lolote litaleta utofauti ndani ya kikosi chake.

Amesema amejipanga vyema kuhakikisha kila mmoja huko Anfield anajisikia mwenye furaha kila panapokucha hivyo hana tatizo la kuhisi kuondoka kwa Torres kutawapa wakati mgumu wachezaji wake pamoja na mashabiki wa Liverpool.

Hata hivyo King Kenny Dalglish amekiri kila mmoja alimpenda na kufurahishwa na mchango wa Torres alioutoa kwa kipindi cha miaka mitatu aliyokaa klabuni hapo lakini hawana budi kufungua ukurasa mpya na kutazama ni vipi wataweza kufikia malengo ya kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.

Kuondoka kwa Torres kumetoa nafasi kwa washambuliaji wengine kusajiliwa klabuni hapo ambao ni Luis Alberto Suárez Díaz aliatokea Ajax Amsterdam pamoja na Andrew Thomas Carroll *"Andy" Carroll* alietokea Newcastle utd.

Wakati huo huo mashabiki wa soka nchini Uingereza wameonyesha kushangazwa na ada ya uhamisho wa mshanbuliaji mpya wa klabu ya Liverpool Andy Carroll ambapo wamedai uhamisho wake haukustahili kuigharimu klabu yake mpya kiasi cha paund million 35.

Mashabiki hao wamesema uwezo wa Andy Carroll katu hauwezi kuufikia uwezo wa Ferdinand Torres lakini ukitazama uhamisho wao umepishana kwa kiasi cha paund million 15 ambazo haziwezi kuthaminishwa na mshambuliaji huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment