KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, February 5, 2011

James Lee Duncan "Jamie" Carragher KUCHEZA KESHO DHIDI YA CHELSEA.


Meneja wa klabu ya Liverpool King Kenny Dalgilish amesema kesho huenda akamuanzisha kikosini beki wa kimataifa toka nchini Uingereza James Lee Duncan "Jamie" Carragher kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Chelsea.

King Kenny Dalgilish ametoa usthibitisho huo baada ya kuulizwa swali na mmoja wa waandishi wa habari huko mjini Liverpool alipokua akiuzungumzia mchezo huo wa kesho ambao utaunguruma magharibi mwa jiji la London.

Amesema beki huyo yupo tayari kupambana baada ya kuwa nje kwa kipindi cha miezi miwili na katika mchezo uliopita dhidi ya Stoke City alikua benchi hivyo naamini kurejea kwake kutanyanyua ari kwa wachezaji wengine kufanya vyema.

King Kenny Dalgilish pia akawazungumzia wap[inznai wake Chelsea kwa kusema wapo sawa kwa hivi sasa baada ya kuwa katika kipindi cha mpito hivyo naamini mpanano wa kesho utakua na upinzani mkali kwa pande zote mbili.

Kwa upande wa Chelsea wao hiyo kesho wamepanfga kumtumia mshambuliaji wao mpya alieweka rikodi ya usajili nchini Uingereza Fernando José Torres Sanz ambae mpka hii leo ameshafanya mazoezi na kikosi cha klabu hiyo kwa muda wa siku nne.

Meneja wa klabu hiyo ya jijini London Carlo Michelangelo Ancelotti ameeleza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba mshambuliaji huyo ana nafasi kubwa ya kumuanzisha katika kikosi cha kwanza na ana iamni atafanya maajabu kwa kusaidiana na wenzake kuhakikisha wanalipiza kisasi cha kufungwa na Liverpool mabao mawili kwa sifuri katika mchezo wa mnzunguuko wa kwanza ligi huku mabao yote yakifungwa na Torres.

Fernando José Torres Sanz nae amepata nafasi ya kuzungumz ana vyombo vya habari na kueleza kuwa yu tayari kucheza upande wa upinzani dhidi ya klabu yake ya zamani ya Liverpool na hakuna chochote ambachop kitakua kipya kwake.

No comments:

Post a Comment