KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, February 5, 2011

SPURS NA NDOTO ZA KUMSAJILI BECKHAM.


Uongozi wa klabu ya Tottenham Hotspurs umesema bado haujakata tama katika suala la kumsajili kiungo wa kimataiofa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ya LA Galax ya nchini Marekani David Joseph Beckham.

Dhamira hiyo ya uongozi wa Spurs, imetangazwa na meneja wa klabu hiyo Harry Redknapp ambapo amesema baada ya kushindwa kufanikiwa kusajili kwa mkopo kiungo huyo sasa wanajipanga kumr5ejesha moja kwa moja jijini London walipozaliwa.

Redknapp amesema kiungo huyo ambae badfo anafanya mazoezi na kikosi chake, mkataba wake na klabu ya LA Galaxy utafiki kikomo mwezi novemba mwaka huu na wanategemea kutumia mwanya huo kutimiza malengo ya kumsajili.

Amesema tayari ameshazungumza na Beckham na amemueleza kwamba suala hilo halitokua na kipingamizi chochote hivyo wanachokisubiri hivi sasa ni kumalizika kwa mkataba wake, hatua mbayo itamfanya kuwa mchezaji huru.

Becks mwenye umri wa miaka 35, anatarajia kuondoka klabuni hapo juma lijalo na kurejea nchini Marekani kujiunga na kikosi cha klabu ay LA Galax tayari kwa maandalizi kamili ya msimu mpya wa ligi.

No comments:

Post a Comment