Uongozi wa shirikisho la soka nchini Algeria umetangaza kuufuta mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo dhidi ya majirani zao Tunisia uliokua umepangwa kuchezwa kati kati ya juma lijalo.
Uongozi wa shirikisho hilo umeeleza kwamba mchezo huo uliokua umepangwa kufanyika siku ya jumatano nchini Algeria hautokuwepo kufuatia viwanja viwili vya nchini humo kuwa katika shughuli nyingine.
Timu ya taifa ya Algeria pamoja na Tunisia walitaka kuutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya michezo ya hatua ya kwanza ya fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 2012 zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea pamoja na Benin.
Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki ulitarajiwa kuwa mchezo wa kwanza kwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Tunisia Ammar Souayah ambae emeteuliwa jana kufuatia hatua ya kuondoka kwa Faouzi Benzarti.
Sababu kubwa ya Faouzi Benzarti kuondoka ni kutaka kuwa huru kama wananchi wengine wa nchini Tunisia, baada ya kushurutishwa kuifanya kazi hiyo na raisi alieachia madaraka Zine al-Abidine Ben Ali na kukimbilia uhamishoni nchini Saudi Arabia.
Akihojiwa na moja ya chombo cha habari nchini Tunisia jana Faouzi Benzarti amesema ilimlazimu kurejea tena kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tunisia mwezi mmoja uliopita kufuatia amri iliyotolewa ikulu na raisi Zine al-Abidine Ben Ali ambae alimlazimisha kwa nguvu za madaraka aliyokua nayo.
No comments:
Post a Comment