Beki na nahodha wa klabu ya Man Utd Gary Alexander Neville ametangaza kustahafu soka baada ya kusota nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kilichopita.
Gary Alexander Neville mwenye umri wa miaka 35, ametangaza hatua hiyo kufuatia majeraha yanayomkabili ambayo ndio chanzo cha yeye kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kilichopita.
Kubwa linalomsumbua mchezaji huyo ni maumivu ya kifundo cha mguu sambamba na tatizo la korodani ambalo limekua likimtokea mara kwa mara anapokua uwanjani.
Hata hivyo Gary Alexander Neville amesema bado ataendelea kuipenda Man utd na atajitahidi kufanya kila jitihada za kuisaidia klabu hiyo kwa ajili ya kupata mafanikio mengi zaidi.
Gary Alexander Neville ametangaza kustahafu soka huku akiacha historia kubwa ndani ya Man Utd kufuatia kucheza michezo 602 toka alipojiunga na klabu hiyo mwaka 1992 na kwa upande wa timu ya taifa amecheza michezo 85.
Historia yake fupi.
1991: Alisaini mkataba wa kukitumikia kikosi cha kwanza cha Man Utd.
1992: Alijumuishwa kikosini kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kombe la UEFA dhidi ya Torpedo Moscow
1995: Alicheza mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la FA na Man utd walipoteza mbele ya Everton
1996: Alikua mmoja wa wachezaji waliochukua vikombe viwili.
1997: Alifunga bao lake la kwanza akiwa dhidi ya Middlesbrough ambao walilazimisha sare ya mabao 3-3.
1999: Alikua mmoja wa wachezaji walioiwezesha Man utd kutwaa vikombe vitatu ndani ya msimu mmoja.
2000: Alitwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya nne huku akifikisha idadi ya 250 aliyocheza akiwa na Man utd.
2003: Alichukuwa ubingwa wa ligi kwa mara ya sita akiwa na Man utd.
2004: Alitwaa ubingwa wa kombe la FA kwa mara ya tatu na kusaini mkataba wa miaka minne.
2005: Alichaguliwa kuwa nahodha wa kikosi.
2010: Alitwaa ubingwa wa pili wa kombe la ligi.

No comments:
Post a Comment