USA
EGYPT
Shiriksiho la soka nchini Marekani limetangaza kutoipelekea timu ya taifa ya nchi hiyo kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa bara la Afrika Misri uliokua umepangwa kufanyika Februari 9 mjini Cairo.
Taarifa iliyotumwa mjini Cairo yalipo makao makuu ya chama cha soka nchini Misri na kusainiwana raisi wa shirikisho la soka nchini Marekani Sunil Gulati imeeleza kwamba timu ya taifa ya nchi hiyo haitozulu nchini Misri kufuatia maandamano ya wananchi yanayoendelea kwa lengo la kumshurutisha raisi Hosni Mubarak aondoke madarakani.
Alipohopjiwa na vyombo vya habari kwa nini wamefikia maamuzi hayo, raisi huyo wa soka nchini Marekani amesema kwamba ni vigumu kuiruhusu timu ilekee nchini Misri ili hali kila mmoja anafahamu zogo linaendelea nchini humo hivyo ni bora mchezo huo ukapangiwa tarehe nyingine.
Hata hivyo Sunil Gulati amewashukuru viongozi wa chama cha soka nchini Misri kwa ushirikiano mkubwa waliowaonyesha katika kipindi chote cha maandalizi ya mchezo huo kimataifa wa kirafiki ambao ulitaka kutumiwa kama sehemu ya maandalizi ya timu ta taifa ya Misri kujiandaa na michezo ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 2012.
Katika michezo hiyo ya awali ya fainali za mataifa ya bara la Afrika timu ya taifa ya Misri imepangwa katika kundi la saba lenye timu za Afria kusini, Niger pamoja na Sierra Leone ambapo katika mchezo ujao mabingwa hao mara tano wa bara la Afrika watacheza na timu ya taifa ya Afrika kusini March 26 kwenye uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg.

No comments:
Post a Comment