Wakati vilabu vya Liverpool, Chelsea na Newcastle Utd vikiwa gumzo katika vyombo mbali mbali vya habari hii leo, huko Spurs hali si shwari kufuatia klabu hiyo kushindwa kuuwahi muda wa usajili na kukamilisha dili la kumnasa kiungo wa kimataifa toka nchini Scotland na klabu ya Blackpool Chalie Adam.
Meneja wa klabu hiyo ya jijini London Harry Redknapp amesema tayari walikua wameshakaribia kumnasa kiungo huyo lakini baadhi ya utaratibu uliowekwa na viongozi wa klabu ya Blackpool uliwachelesha kutimiza lengo lao.
Amesema hadi mishale ya saa tano usiku mazungumzo kati ya pande hizo mbili yalikua yanaendelea na tayari vyombo mbali mbali vya habari vilikuwa vinafahamu suala usajili wa kiungo huyo lakini wanahisa wawili wa klabu ya Blackpool walichelewa kutia saini katika makubaliano ya uhamisho wake.
Hata hivyo alipoulizwa mtendaji mkuu wa klabu ya Backpool Owen Oyston amekiri ni kweli mazungumzo ya kumuuza Chalie Adam yalikua yakiendelea usiku wa kumkia hii leo lakini hayakufikia muafaka na wala hawakua karibu kumruhusu kuondoka kwani tayari kulijitokeza dosari za kiutendaji.
No comments:
Post a Comment