Uongozi wa klabu ya Newcastle Utd umethibitisha kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Finland Shefki Kuqi kwa kipindi cha miezi mitano ijayo.
Shefki Kuqi ambae tayari ameshawahi kuvitumikia vilabu vya ligi kuu ya soka nchini Uingereza kama Blackburn Rovers pamoja na Fulham amekamilisha safari ya kurejea kwenye ligi hiyo akiwa kama mchezaji huru kufuatia mkataba wake na klabu ya Swansee kufikia kikomo mwaka 2010.
Kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo ni sehemu ya kuziba nafasi zilizoachwa wazi huko Newcastle Utd hivyo inaaminika kwamba Kuqi, mwenye umri wa miaka 34, atatumia uzoefu alionao kuhakikisha anasaidiana na wenzake kufanya kweli msimu huu.
Akizungumzia safari yake ya kurejea tena kwenye mikiki mikiki ya ligi kuu ya Uingereza Shefki Kuqi amesema hawezi kuelezea furaha aliyonayo zaidi ya kusubiri kuanza kuitumikia klabu yake mpya ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya kumi kwenye msimamo wa ligi.
Amesema kabla ya kukamilisha utaratibu wa kuekekea St James Park, alifanya mkutano na meneja wake kwa sasa Alan Pardew na amemuelezea sababu kadha wa kadha ambazo zilimvutia kumsajili ambapo sababu kubwa aliyoitoa ni kumfahamu vyema toka siku za nyuma na aliku akimfuatilia kwa kipindi kirefu kilichopita.
Shefki Kuqi anatarajiwa kuwepo kwenye kikosi kitakachocheza mwishoni mwa juma hili dhidi ya Fulham huko Craven Cottege, huku akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Shola Foluwashola Ameobi anaesumbuliwa na maumivu ya ugoko.
Licha ya kusajiliwa Shefki Kuqi, Newcastle Utd bado wanaripotiwa kuendelea na mawindo ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa klabu za Arsenal pamoja na Middlesbrough Jeremie Aliadiere sambamba na winga wa kibrazil alietemwa na klabu ya Palmeiras Ewerthon Henrique de Souza.
No comments:
Post a Comment