Uongozi wa klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki unajipanga kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast pamoja na klabu ya Chelsea Salomon Armand Magloire Kalou kwa ada ya uhamisho wa paund million 9.
Uongozi wa klabu hiyo umejipanga kufanya hivyo mwishoni mwa msimu huu kufuatia mipango ya benchi la ufundi la klabu ya Chelsea, kumuweka pembeni Solomon Kalou ambae kwa sasa ana nafasi finyu ya kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza kufuatia kusajiliwa kwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando Torres mwishoni mwa mwezi uliopita.
Hata hivyo mipango ya benchi la ufundi la klabu ya Chelsea imelazimika kumuweka pembeni mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kufuatia shinikizo kutoka kwa mmiliki Roman Abramovich ambae anasuka mipango ya kujenga upya safu ya ushambuliaji klabuni hapo.
Mbali na Solomon Kalou kuhusishwa na taarifa za kuwa mbioni kuondoka mwishoni mwa msimu huu pia kuna wachezaji wengine yasemekana wapo kwenye mkumbo huo wa kuondoka kama Didier Yves Drogba Tébily pamoja na John Michael Nchekwube Obinna *Obi Mikel*.
No comments:
Post a Comment