KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, February 1, 2011

YALIKUA MAAMUZI YA KIJASIR I!!!


Baada ya kukamilika kwa safari ya kutoka mjini Liverpool na kutua mjini London usiku wa kuamkia hii leo mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando José Torres Sanz amesema amefanya chaguo lililo sahihi kujiunga na klabu ya Chelsea na kuondoka Liverpool alipodumu kwa kipindi cha miaka miatatu iliyopita.

Torres mwenye umri wa miaka 26 amesema anajisikia mwenye furaha baada ya kutimiza lengo hilo ambalo sasa ameahidi kulifanyia kazi kwa vitendo huku akitoa ahadi nyingine ya kuhakikisha anaisaidia klabu yake mpya kurejesha heshima katika kipindi cha kuelekea ukingoni mwa msimu wa ligi.

Amesema yalikua ni maamuzi magumu kwake na familia yake pia kwani aliipenda sana Liverpool kutoka moyoni lakini, alikua hana namna ya kukubaliana na utaratibu huo ambao hii leo umemfanya kuwa mchezaji halali wa klabu ya Chelsea.

Mshambuliaji huyo ambae ameacha historia ya kuitumikia klabu ya Liverpool katika michezo 142 na kufunga mabao 81 Amesema anajua wengi watachukizwa na maamuzi hayo lakini amewataka radhi kwa kile alichokikusudia na kukitimiza usiku wa kuamkia hii leo na amewataka watu wa Chelsea kunzia kwa viongozi, wachezaji pamoja na mashabiki kumuonyesha ushirikiano wa kutosha ili kuweza kufanikisha malengo yaliyowekwa huko Stamforde Bridge.

Torres amejiunga na klabu ya Chelsea baada ya kuhusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu hiyo kwa vipindi tofauti tofauti vya misimu kadhaa iliyopita, lakini yeye binafsi alitoa kauli ya kuwa tayari kuelekea Stamford Bridge mwishoni mwa juma lililopita baada ya uongozi wa klabu ya Liverpool kuikataa ofa ya paund million 40.

Usajili wake kutoka Liverpool umeigharimu klabu ya Chelsea kiasi cha paund million 50 ambacho kiliainishwa wazi katika mkataba wake na The reds.

Wakati Torres akikamilisha dili la kujiunga na The Blues, nae beki wa kimataifa toka nchini Brazil David Luiz amefanikisha usajili wa kujiunga na klabu hiyo wa mjini London kwa ada ya uhamisho wa paund million 21.4 akitokea katika klabu ya Benfica ya nchini Ureno.

Kufuatia hatua hiyo mwenyekiti wa klabu ya Chelsea Bruce Burk amesema kiujumla uongozi wa klabu ya Chelsea ukiongozwa na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich umefurahishwa na kasi ya usajili ilivyokwenda ndani ya dakika za mwisho na kutimiza malengo ya kuwasajili wachezaji hao wawili.

Kwa ujumla Chelsea imetumia kiasi cha paund million 71.4 ndani ya usiku mmoja ambazo zimetumika kukamilisha usajili wa wachezaji hao wawili ambao tayari imeshasemekana huenda wakajumuishwa kikosini mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa ligi dhidi ya Liverpool.

No comments:

Post a Comment