Mshambuliaji mpya wa klabu ya Liverpool Andrew Thomas Carroll *Andy Carroll* amesema haikuwa dhamira yake kuondoka huko St James Park katika kipindi cha dirisha dogo la usajili kilichofikia tamati usiku wa kuamkia hii leo.
Andy Carroll ametoa kauli hiyo saa kadhaa baada ya uhamisho wake kukamilika huko Anfield ambao umeigharimu klabu ya Liverpool kiasi cha paund million 35.
Amesema lengo lake kubwa lilikua ni kutaka kuendelea kuitumikia klabu ya Newcastle utd kwa kipindi kirefu kufuatia mapenzi aliyokua nayo lakini ilimemlazimu kuondoka baada ya uongozi wa klabu hiyo kuikubali ofa ya paund million 35 iliyotumwa kutoka Anfield.
Mshambulaiji huyo mwenye umri wa miaka 22 ameendelea kueleza kwamba hatua ya kuipenda Newcastle Utd ilifahamika hadi kwa mashabiki wa klabu hiyo hivyo imekua vigumu kwake kufanya maamuzi ya kuondoka huku akikiria amewakera mno mashabiki wa The Magpies ambao walimpa ushirikiano mkubwa toka alipoanza kuitumikia klabu hiyo mwaka 2006.
Hata hivyo mshabiki wa klabu ya Newcaste Utd usiku wa kuamkia hii leo walionekana kupigwa na bumbuwazi kufuatia uhamisho wa mshambuliaji huyo ambapo miongoni mwao wamesema hawakuratajia kama Andy Carroll angeweza kuondoka katika himaya ya klabu yao huku baadhi yao wakiwalaumu viongozi wao kwa kukubali kirahisi kumuuza mshambuliaji huyo.
Wakati mashabiki wa soka mjini Newcastle wakionyesha kuhuzunishwa na hatua ya mshambuliaji Andy Carroll kuondoka kwenye himaya yao, meneja wa klabu hiyo Alan Scott Pardew amepasua ukweli wa nini kilichomuondoa mshambuliaji huyo.
Alan Scott Pardew amesema Andy Carroll kwa kipindi kirefu alikua katika mjadala wa kusaini mkataba mpya lakini cha kushangaza alikua akihimiza suala hilo litimizwe na kama litashindikana katika kipindi cha siku kadhaa zilizopita ataomba uhamisho na kujiunga na klabu nyingine.
Meneja huyo alichukua nafasi ya Criss Hughton mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana ameendelea kueleza wazi kwamba alidiriki kusema mchezaji huyo hatouzwa katika kipindi cha dirisha dogo kwa minajili ya kuutaka uongozi uharakishe mkataba mpya lakini suala hilo lilichelewesha na usiku wa kuamkia hii leo Carroll ametimiza lengo lake la kuondoka.
Andy Carroll alianza kuitumikia klabu ya Newcastle mwaka 2006 na mpaka anaondoka klabuni hapo usiku wa kuamkia hii leo tayari alikua ameshacheza michezo 80 na kupachika mabao 31.
Katika msimu wa mwaka 2007-208 mshambuliaji huyo aliuzwa kwa mkopo kwenye klabu ya Preston North End ambapo huku alifanikiwa kucheza michezo 11 na kupachika bao moja.
Kusajiliwa kwake Liverpool kunatarajiwa kutengeneza ushirikiano kati yake na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uruguay Luis Alberto Suárez Díaz aliesajiliwa akitokea Ajax Amsterdam.
No comments:
Post a Comment