Bao lililofungwa katika dakika ya 8 na mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Uingereza na klabu ya Arsenal Alex Chamberlain, limemfanya mchezaji huyo kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo aliefunga kupitia michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Alex Chamberlain aweka rekodi hiyo na kuvunja rekodi iliyokua inashikiliwa na kiungo wa klabu ya arsenal Theo Walcot ambae mwaka 2007 alipata nafasi ya kufunga bao katika michuano hiyo akiwa na umri wa miaka 18 na siku 221.
Alex Chamberlain ambae kwa sasa ana umri wa miaka 18 na siku 44, amesema amefarijika na hatua hiyo ambayo anaamini imekuja kutokana na juhudi zake pamoja na ushirikiano na wachezaji wengine waliokuwepo kikosini hiyo jana.
Amesema mbali na suala hilo pia hana budi kuwashukuru wale wote waliomuwezesha kufikia mafanikio ya kucheza katika klabu kubwa inayotambulika ulimwenguni kote hatua ambayo imemfanya acheze katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo jana ulikua mchezo wake wa kwanza.
Alex Chamberlain 18 yrs 44days..Olympiacos ...2011.
Theo Walcot 18 yrs 221 days.. Slavia Prague ...2007.
Jack Wilshare 18 yrs 291 days.. Shakhtar Donetsk...2010.
Rooney 18 yrs 340 days..Fenerbahce..2004.
Bekham 19 yrs 219 days.
Nae meneja msazidi wa klabu ya Arsenal Pat Rice ambae jana alikua mkuu wa benchi la ufundi kufuatia bosi wake Arsene Wenger aliemaliza adhabu ya kufungiwa michezo miwili na UEFA amesema ni jambo zuri kwa mchezaji mwenye umri mdogo kama Alex Chamberlain kupata mafanikio hayo.
Amesema ni mara chache sana kwa wachezaji kama winga huyo kufunga kwenye michuano mikubwa kama ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hivyo bado akaendelea kusisitiza jambo la kufarijika na muonekano wa kikosi alichokipanga hiyo jana dhidi ya mabingwa wa soka toka nchini Ugiriki, Olympiacos ambao walikubali kibano cha mabao mawili kwa moja.
Bao la pili la Arsenal lilifungwa na beki wa pembeni kutoka nchini Brazil Andre Santos aliesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea katika klabu ya Fenabahce ya nchini Uturuki huku bao la kufutia machozi la olympiacos likifungwa na David Fuster.
No comments:
Post a Comment