KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 29, 2011

Frank Lampard AKIRI KUKASIRIKA.

Mfungaji wa bao la Chelsea katika mchezo wa kundi la tano la michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Valencia CF uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo huko Stadio Mestella Frank Lampard amekiri hakufurahishwa na hatua ya kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast Solomon Kalou.

Frank Lampard amesema alistahili kuendelea kubaki kikosini kwa ajili ya kuongeza purukushani za kusaidiana na wengine katika harakati za kusaka ushindi wakiwa ugenini lakini mwisho wa siku walijikuta wakilazimishwa sare ya bao moja kwa moja.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, amesema kwamba mchezo wa jana ulikua mzuri sana kwake kutokana na uchezaji mzuri wa kikosi cha Chelsea ulioonyeshwa uwanjani na alidhani angemaliza katika dakika zote 90.

Hata hivyo amedai kwamba anaheshimu maamuzi ya meneja Andre Villas Boas ambae ndie mwenye jukumu la kuamua nani acheze tena kwa wakati gani na mchezo gani katika msimu mzima wa soka.

Katika hatua nyingine meneja wa klabu ya Chelsea Andre Villas Boas ameonyesha kufurahishwa na mpango wake wa kumjumuisha kikosini Frank Lampard katika mchezo dhidi ya Valencia CF.

Andre Villas Boas amesema mashabiki wengi walikua wanambeza kiungo huyo kwa kisingizio cha kushikwa kwa kiwango chake ambapo anadhani hali hiyo ilitokana na kutompanga katika michezo kadhaa iliyopita.

Amesema hatua ya kufunga bao katika mpambano huo imekuwa nzuri kwake na pia imekuja kwa wakati muafaka baada ya kuwatahadharisha mashabiki wanaombeza Frank Lampard.

No comments:

Post a Comment