
Uongozi wa klabu ya Chelsea umemteua Frank Arnesen kuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo kwa lengo la kumsaidia meneja wa kikosi cha kwanza Carlo Ancelotti.
Arnesen anatwaa cheo hicho kwa kupanda daraja toka mkurugenzi wa benchi la Mascout ambao wamekuwa wakifuatilia vipaji vya wachezaji mbali mbali ulimwenguni kote ili waweze kujiunga na klabu hiyo.
Taarifa toka ndani ya klabu ya Chelsea imeeleza kuwa pamoja na Arnesen kuteuliwa kushika wadhifa huo bado ataendelea kuliisaidia jopo na Mascout klabuni hapo.
Hata hivyo taarifa hizo imeeleza kwamba uongozi wa klabu ya Chelsea umefikia maamuzi hayo kwa kuamini mchango wa Arnesen utaweza kumpa nafasi Carlo Ancelotti kukiongoza vyema kikosi chake katika msimu mpya wa ligi.
Arnesen alijiunga na klabu ya Chelsea mnamo mwaka 2005 akitokea katika klabu ya Tottenham, na mwezi May mwaka huu wa 2009 aliungana na bodi ya wakurugenzi wa The Blues.
No comments:
Post a Comment