KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 13, 2009

MAN CITY WAKATA TAMAA !!!!!!!!!

Klabu ya Man City imeonekana kukatishwa tamaa na utaratibu wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Cameroon na klabu ya Barcelona Samuel Eto'o.

Man City wameonekana kuwa katika hali hiyo kufuatia kutoona utaratibu wowote wa kukubaliwa kwa ofa yao ya paund million 25 waliyoituma huko Nou Camp majuma kadhaa yaliyopita.

Akizungumza na vyombo vya habari hii leo, mtendaji mkuu wa klabu ya Man City Garry Cook amesema utaratibu unaoendelea kuonekana mbele yao unaonyesha dhahir hawatoweza kukamilisha dili la kumpata mshambuliaji huyo.

Cook amesema kwa upande wao hawana tatizo la kukamilisha usajili huo lakini upende wa pili wa Barcelona unaonekana kuwa na matatizo ya kutoa maamuzi kama wanamuuza Eto’o ama la, hali ambayo inawakatisha tamaa kila muda unavyosogea.

Endapo dili hilo la Eto'o la kuelekea huko Eastlands litakamilika, uongozi wa klabu ya Man City umesema upo tayari kumlipa mshahara wa paund laki 2 na nusu kwa juma, mshahara ambao utakuwa mkubwa kuliko wa mchezaji yoyote ulimwenguni anaecheza soka.

Ikumbukwe kuwa Eto'o alisajiliwa na klabu ya Barcelona kwa gharama ya paund million 16 akitokea Real Mallorca mnamo mwaka 2004 na mpaka sasa mshambuliaji huyo toka nchini Cameroon ameshaifungia klabu hiyo zaidi ya mabao 100 ndani ya misimu mitato aliyokaa huko Nou Camp.

Sifa nyingine ya mshambuliaji huyo ni kuwa chachu ya kuisaidia Barcelona kutwaa vikombe vitatu msimu uliopita ambapo miongoni mwa vikombe hivyo ni pamoja na michuano ya kombe la mfalme, ligi kuu ya soka nchini Hispania pamoja na kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Man City mpaka sasa wameshafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Paraguay Roque Santa Cruz aliekuwa Bluck Burn rovers kwa kiasi cha paund million 18 pamoja na kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza Gareth Barry aliekuwa Aston Villa kwa kiasi cha paund million 12.




No comments:

Post a Comment