KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 17, 2009

MILANGO IWAZI KWA ALBERTO AQUILANI.


Uongozi wa klabu ya As Roma umekubali kufungua milango ya kuwawezesha Liverpool kutuma ofa ya kumsajili Alberto Aquilani.


Aquilani amekuwa akiripotiwa kuwa mbioni kusajiliwa na klabu ya Liverpool lakini uongozi wa klabu yake ulikuwa ukikanusha taarifa hizo kwa kuuelezea umma kwamba mchezaji huyo kamwe hatouzwa.


Meneja wa klabu ya AS Roma Luciano Spalletti amesema kwa sasa hana lolote la kuzungumza juu ya kuondoka ama kubaki kwa Aquilani, lakini akasisitiza kwamba njia ni nyeupe kwa mchezaji huyo kufikiria kama ataendelea kusalia Stadio Olympico msimu ujao ama la.


Kwa upande wake mkurugenzi wa klabu ya AS Roma Bruno Conti amethibitisha kuwepo kwa taratibu za klabu ya Liverpool kutaka kutuma ofa ya kutaka kumsajili mchezaji huyo hali ambayo amekubaliana nayo kwa kusema endapo ofa hiyo itawafikia wataifanyia kazi.


Aquilani, mwenye umri wa miaka 25, bado ana mkataba wa kuichezea klabu ya AS Roma mpaka mwezi June mwaka 2013.




No comments:

Post a Comment