KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 6, 2009

DIDIER DROGBA KUSALIA DARAJANI.

Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast DIDIER DROGBA amekubali kuongeza mkataba wa miaka miaka mitatu katika mkataba wake wa sasa ambao utamuwezesha kuendelea kuichezea klabu hiyo kwa mshahara wa paundi laki moja kwa juma.

Makubaliano hayo yanataraji kuwekwa hadharan siku chache zijazo baada ya wawakilishi wa mshambuliaji huyo kufikia makubaliano hayo ambayo yanampa nguvu zaidi meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya nchini Uingereza.

Makubaliano hayo yamehitimisha sintofahamu ya Drogba kuendelea kubaki jijini London katika makao makuu ya klabu Chelsea huko Stamford Bridge mara baada ya kumlaumu hadharani mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.

Itakumbukwa kuwa Drogba mwenye umri wa miaka 30 alikorofishana na aliyekuwa meneja wa klabu hiyo Luis Philipe Scolari mapema msimu uliopita kwa kile alichodai meneja huyo alikuwa hampi haki ya kumjumuisha katika kikosi chake mara kwa mara.

Utovu wa nidhamu wa mshambuliaji huyo uliendelea msimu uliopita kwa kumshambulia hadharani mwamuzi Henning Ovrebo katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mbingwa barani ulaya dhidi ya klabu ya Barcelona.

No comments:

Post a Comment