KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 5, 2009

WAGONGA NYUNDO WAKWAMA !!!!!!!!!!


Uongozi wa klabu ya Bayern Munich umevunja mazungumza na uongozi wa klabu ya West Ham Utd ya nchini Uingereza ambayo ilikuwa inataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Italia pamoja na klabu hiyo ya Ujerumani Luca Toni kwa mkopo.


Taarifa za kuvunjwa kwa mazungumzi hayo zimetolewa na mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Bayern Munich Christian Nerlinger.


Hatua za kufanywa mazungumzo hayo ya kutaka kumuuza kwa mkopo Luca Toni zimekuja kufuatia hatua ya kusajiliwa kwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ujerumani Mario Gomez na mashambuliaji wa kimataifa toka nchini Croatia Ivica Olic ambao wanapewa nafasi ya kuwepo katika kikosi cha kwanza cha Bayern Munich msimu ujao.



1 comment:

  1. Hakika ni faraja kuwa umerejea. Naamini wengi wamepata mengi leo.
    Blessings

    ReplyDelete