Klabu za Liverpool na Real Madrid bado zinaendelea na mazungumuzo kuhusu uhamisho wa kiungo Xabi Alonso.Viongozi wa vilabu hivyo jose angel sanches wa real Madrid na christen purslow wa Liverpool wamekutana mjini Barcelona kuzungumzia uhamisho huo.
Klabu ya Madrid ipo tayari kulipa paundi million 30 kama ada ya uhamisho, kiasi ambacho ni pungufu ya paundi million 5 kukamilisha ada ya paundi milioni 35 zinazohitajika na klabu ya Liverpool ili wamuachie kiungo huyo.
Hata hivyo inaelezwa kuwa iwapo klabu hizo mbili hazitafikia makubaliano, klabu ya Real Madrid itaanza mikakati ya kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini ubelgiji Steven Defour anayechezea klabu ya Standard Liege.
Kwa upande wake Alonso amesema anataka mazungumzo hayo yafanyike na uamuzi ufikiwe haraka.
Mpaka sasa klabu ya Real Madrid imetumia kiasi cha paundi milioni 200 kusajili wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya soka nchini Hispania ambapo wachezaji hao waliosajiliwa ni Cristiano Ronaldo , Karim Benzema na Kaka.
Pia kuna taarifa kuwa Madrid wamefikia makubaliano na klabu ya inter Milan waliotayari kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini uholanzi Wesley Sneider kwa ada ya paundi milioni 18.
Samahani wewe unaetupasha hizi habali,nina swali la kizushi,hivi kombe la Hispania linasimamia galama ya paunti au dola ngapi,au kombe la uingereza,na kombe la ulaya?asante kwa jibu.mdau wa Japani.
ReplyDelete