KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 4, 2009

ARSENAL WAKARIBIA KWA KALOU.


Klabu ya ARSENAL inakaribia kumnasa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast na klabu ya Chelsea Salomon Kalou.

Washika bunduki hao wa jijini London wametuma kiasi cha paund million 6 kwa lengo la kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, lakini kiasi hicho kimekataliwa na The Blues ambao tayari wameainisha bei ya kuuzwa kwa mchezaji huyo kuwa ni paund million 8.


Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger yu tayari kumlipa mshambuliaji huyo mshahara wa paund elfu 60 kwa juma endapo tafanikiwa kumsajili ndani ya kikosi chake.

Kalou mwenyewe amevieleza vyombo vya habari kwamba ni hatua nzuri kwake kutarajia kuwa chini ya meneja ambae anafahamu namna ya kumtunza mchezaji.

No comments:

Post a Comment