KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, November 27, 2009

BADO NI KIZUNGUMKUTI.


Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene wenge ameshindwa kutoa taarifa kamili za beki wake wa kimataifa toka nchini Ufaransa William Gallas kama ataweza kucheza mchezo wa jumapili dhidi ya Chelsea ama la, kufuatia jeraha la jicho alilolipata siku mbili zilizopita kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Standard Liege toka nchini Ubelgiji.

Wenger amesema hafahamu kama beki huyo ataweza kucheza ama kutokucheza lakini mpaka sasa bado ana uvimbe katika jicho lake la upande wa kulia ambao umepelekea kutokuona vizuri.

Hata hivyo meneja huyo amesema bado kuna muda wa kuangalia kama beki huyo atacheza mchezo huo wa jumapili hivyo si vyema sana kumzungumzia kwa sasa ili hali jopo la madktari likiendelea kufanya kazi yao.

No comments:

Post a Comment