Hatua hiyo huenda ikaivutia klabu ya Barcelona yenye lengo la kumsajili beki huyo wa kimataifa toka nchini Serbia licha ya kuwa wakala wake anataka mteja wake aongeze mkataba.
Mbali na Vidic, wachezaji wengine nyota wa klabu ya Manchester United hawataongezewa posho zao mpaka watakapobakiza mwaka mmoja katika mikataba yao lengo likiwa ni kuepuka hasara inayoweza kuipata klabu kama mchezaji ataamua kuondoka Old Trafford huku akiwa bado ana mkataba.
Mpaka mwishoni mwa msimu huu Vidic atakuwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa ambao unamuwezesha kulipa paundi elfu 70,000 kwa juma.
Vidic aliyesajiliwa kutoka klabu ya Spartak Moscow kwa ada ya paundi milioni saba mwezi January 2006 alitarajia kuongeza mkataba ambao ungemwezesha kulipa posho ya paundi laki 1 .
Hata hivyo amesema bado anafuraha kuendelea kuichezea klabu hiyo na asingependa kuzungumzia hatma yake mapema .
Awali klabu hiyo ilikuwa inaanza kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba na wachezaji wanapokuwa wamebakiza miaka miwili katika mikataba yao lakini wamiliki wa klabu hiyo familia ya Glazers imeona hakuna umuhimu wa kuanza kuzungumza na mchezaji kuhusu suala la kuongeza mkataba akiwa bado ana miaka miwili iliyosalia katika mkataba wa awali .

Sera hiyo imeiwezesha klabu ya Manchester kubana matumizi na kufanikiwa kulipa madeni ambapo klabu hiyo ina deni linalofikia paundi milioni 690.
No comments:
Post a Comment